|
|
Watu mia moja na nne, waume, wanawake na watoto walipanda ndege aina ya MI 185
tarehe19 Desemba 1997 kutoka Jakarta.
Wakati ndege ilipokuwa ikinapaa kuelekea Singapore, hakuna hata mmoja wao
aliyeweza kujua kuwa hawatafika mwisho wa safari yao. Ndege yao Boeing 737 aina ya
Jeti ghafla karibu na Palembong ilipiga mbizi na kupasuka vipande vipande karibu na
Sungei Musi, na kuua abiria wote pamoja na wafanyikazi wote wa ndege hiyo.
Watu wote duniani wanapata majanga makubwa ya vifo, matetemeko ya ardhi,
vimbunga, ajali mbali mbali. Hayo ni mifano ya majanga yanayo kuja ghafla bila
kutegemea, hivyo watu wanakuwa hawana uwezo wa kudhibiti vifo vya namna hiyo.
Watu wengine wanakufa kutokana na magonjwa yasiyotibika. Kila mmoja wetu
anajaribu kujitayarisha kwa ajili ya kifo, lakini kifo siku zote hakitabiriki na
hakidhibitiwi.
Baadhi ya watu wanajaribu kuishi maisha marefu kwa kutovuta sigara na kufanya
mazoezi ya viungo, kula vyakula bora, pamoja na kunywa vidonge vyenye kuongeza afya
(vitamini). Pamoja na hayo, hatuwezi kukataa ukweli kuwa siku moja tutakufa.
Watu wengine hawafikirii kuhusu kifo, wakati wanapokuwa hawakabiliwi na matatizo,
wakati wanapokuwa na uwezo wa kuwa na chakula na fedha, wakati hakuna matatizo ya
kifamilia na wanapokuwa na nafasi/ cheo katika jamii, kifo kinakuwa mbali na mawazo
yao. Lakini kifo hakifiki kwa watu wazeena wenye shida tu, pia watu wenye akili na
vijana wanaweza kufa bila taarifa. Kifo kinaleta usawa kwa wote tokia tabaka kwa juu
hadi tabaka ya chini.
Mungu, ana madaraka ya kutuweka mbinguni na kutuhukumu jehanamu kulingana na
hukumu yake. Jina lake Ar Rahmani Rahim [yeye Masiha na mkamilifu] hivyo
anatuonya tujihadhari na kujitayarisha wakati wote kwa kifo na kiama . Kila mtu atakufa
siku mmojana badaye kuhukumiwa siku ya hukumu, wakati kila moja atahukumiwa
kutokana na matendo yake aliofanya wakati wa maisha yake duniani
Hivyo Mungu anatutaka, tuwe tayari muda wotekuanzia sasa. Aliye tayari wakati
wowote ni yule anaye tembeya katika njia iliyo nyoofu katika amani ambayo Mungu
pekee ndiye anatoa.
|
|